Maelezo ya Ufaragha (Privacy Statement)

Utangulizi

Serikali ya British Columbia (B.C.) na United Way ya British Columbia (United Way BC) inajitahidi kulinda ufaragha wako. Serikali ya B.C. na United Way BC zinakusanya, zinatumia na kuweka wazi taarifa zako binafsi kwa mujibu wa Sheria ya Uhuru wa Taarifa na Ulinzi wa Faragha (FOIPPA) na sheria zingine zinazohusika. ‘Taarifa binafsi’ inaainishwa kwa mapana katika sheria ya Uhuru wa Taarifa na Ulinzi wa Faragha kama Taarifa iliyorekodiwa kuhusu mtu anayetambulika, zaidi ya taarifa za mawasiliano, ambazo ndizo taarifa zilizotumika kuwasiliana na mtu mahala pa kazi. Makusudi ya taarifa ya faragha ni kukujulisha kuwa taarifa binafsi ambazo zinaweza kukusanywa kutoka wakati unazuru tovuti ya Kitengo cha Usaidizi wa Simu kwa Matukio ya Ubaguzi wa Rangi na jinsi hizo taarifa zinaweza kutumika.

Upeo

Taarifa hii ya faragha inahusiana tu na habari ambazo zimekusanywa moja kwa moja kutoka kwako ikiwa ni matokeo ya kuzuru tovuti. Haijumuishi taarifa uliyoulizwa na tovuti. Nyongeza yoyote ya taarifa binafsi iliyokusanywa na tovuti itajadiliwa katika taarifa ya ukusanywaji kwenye tovuti hiyo.

Taarifa binafsi zangu zinakusanywaje?

Tovuti ya serikali ya B.C. inakusanya taarifa kuhusu uzuru wako, kujumuisha taarifa binafsi, kwa kutumia kumbukumbu za ukaguzi na vidakuzi. Kidakuzi ni faili ndogo lililotunzwa kwenye kompyuta yako na kivinjari wakati unatumia tovuti.

Ni taarifa binafsi gani zinazokusanywa?

Taarifa zinazokusanywa ni:

Kupitia tovuti zake, Serikali ya B.C., itakutaarifu kama vidakuzi vitakuwa vinakusanya taarifa zaidi kutoka kwako. Kidakuzi kinaweza kubaki kwenye kompyuta yako baada kipindi cha mtandao kuisha (mpaka muda wa kidakuzi unapoisha au umekifuta).

Serikali ya B.C. na United Way BC hukusanya taarifa binafsi chini ya mamlaka ya kipengere 26(c) cha FOIPPA kwa makusudi yaliyoelezwa hapo chini kwenye sehemu inayofuata.

Nini makusudi ya kukusanya taarifa binafsi zangu na zitatumikaje?

Serikali ya B.C. na United Way BC zinakusanya taarifa binafsi kupitia vidukuzi ili kuelewa vema mienendo ya jumla ya mtumiaji na kuboresha utendaji wa mtandao. Taarifa binafsi zitatumiwa tu na mfanyakazi anayeruhusiwa kutimiza makusudi yaliyotumika awali kukusanya au kwa matumizi sambamba na makusudi hayo, vinginevyo isipokuwa kama unakubali waziwazi. Serikali ya B.C. na United Way BC hukusanya taarifa binafsi kupitia ukaguzi salama kulinda zidi ya vitisho kutoka kwa wadukuzi, na kwa ajili ya utekelezaji mwingine na usalama. Serikali ya B.C. na United Way BC hawatumii takwimu kuamua utambulisho wako, labda iwe inatakiwa kama sehemu ya uchunguzi wa ndani au kwa utekelezaji wa sheria nyingine, na hapo itakuwa katika kufuata FOIPPA.  

Naweza kujitoa kukusanywa taarifa binafsi?

Kivinjari chako kinaweza kukuruhusu kulemaza vidakozi, lakini huwezi kujitoa kwenye ukusanyaji wa taarifa binafsi zinazokusanywa kwa makusudi ya ukaguzi. Vile vile, uamuzi wako kulemaza vidakozi unaweza ukaathiri uwezo wako wa kuvinjari mtandaoni, kusoma, na kupakua taarifa zilizo kwenye tovuti ya Serikali ya B.C., na serikali inaweza ikashindwa kubinafsisha uzoefu wako wa mtandaoni. Lakini, bado unaweza kupata huduma za Serikali ya B.C. kwa njia nyingine kama vile mawasiliano ya ana kwa ana, faksi au barua pepe.

Kuna ulinzi gani uliowekwa kulinda taarifa binafsi?

Serikali ya B.C. na United Way BC wanawajibika kulinda tarifa zako binafsi kwa kuweka mipango ya usalama inayofaa dhidi hatarishi kama vile muingilio ambao hakuruhusiwa, kukusanya, kutumia, kuweka wazi au utupwaji. Zaidi hasa, mwiingilio wa mfumo, matumizi na ukusanyaji wa taarifa unaruhusiwa tu kwa wafanyakazi wenye kibali. Zaidi, taarifa binafsi zozote zilizokusanywa na kutumiwa kutambua miendelezo ya mtumiaji (kama vile anuani ya IP) inakusanywa katika ngazi ya jumuisho na kufanywa isitambulike imetoka kwa nani wakati wa kuunda ripoti.

Taarifa zinahifadhiwa kwa muda gani?

Baadhi ya vidakuzi vitabaki kwenye kompyuta yako kwa muda ambao kivinjari chako kiko wazi, au mpaka umevifuta kutoka kwenye kompyuta yako. Vidakuzi vingine vitabaki kwenye kompyuta yako ili uweze kutambulika utakaporudi kwenye tovuti. Muda wa vidakuzi hivi utaisha siyo zaidi ya miezi 18 tangu vilipowekwa kwenye kompyuta yako mara ya kwanza. Taarifa zilizokusanywa kama sehemu ya kidakuzi au logi ya ukaguzi wa usalama zinatunzwa kwa miaka 2. Taarifa zilizokusanywa au kuundwa na Serikali ya B.C. zinatunzwa kwa mujibu wa  ratiba ya uhifadhi wa kumbukumbu za serikali na mahitaji mengine ya kisheria.

Nawezaje kufikia na kusahihisha taarifa nilizotuma kwenye tovuti?

Unaweza kuhakiki taarifa binafsi yoyote iliyokusanywa kuhusu wewe kwa kuomba kibali kutoka wizara inayotunza taarifa hizo, au kwa kuwasilisha ombi la Uhuru wa Habari. Unaweza Ukaomba mabadiliko au nyongeza kwenye taarifa zako binafsi kama unaamini kuwa kuna mapungufu kwa kupeleka maombi ya maandishi ukieleza mapungufu hayo. Tafadhali wasiliana na wizara au taasisi nyingine za serikali zinazoshikilia taarifa zako binafsi. Tawi la Faragha, Uzingatiaji na Mafunzo linaweza kufikiwa kwa taarifa za kawaida.

Yupi naweza kuwasiliana naye kuhusu haya maelzo ya ufaragha?

Maswali kuhusu maelezo haya ya ufaragha, pamaoja na ukusanywaji wa taarifa binafsi, yanaweza kuelekezwa kwa Mshauri Mkuu wa Faragha kwenye Tawi la Faragha, Uzingatiaji na Mafunzo lilopo kwenye Wizara ya Fedha, Sanduku la Posta 9493 Stn Prov Govt, Victoria, BC., V8W 9N7, simu 250-356-1851. Privacy.Helpline@gov.bc.ca.