Msaada uko hapa
Ikiwa wewe au mpendwa wako mmekumbwa au kushuhudia ubaguzi wa rangi ndani ya British Columbia, msaada unapatikana.
Wapigie simu Kitengo cha Usaidizi wa Simu kwa Matukio ya Ubaguzi wa Rangi uongee na mtaalamu mwenye mafunzo ambaye atakusaidia kupitia rasilimali zinazopatikana katika jumuiya yako.
Inapatikana Jumatatu hadi Ijumaa 9:00 asubuhi hadi 5:00 jioni (PT)
Haina malipo, ni ya usiri na inapatikana katika lugha 240.
Kitengo cha Usaidizi wa Simu kwa Matukio ya Ubaguzi wa Rangi hakikusudiwi kuchukua nafasi ya huduma za dharura. Ikiwa uko katika shida ya haraka au hatari, piga simu 911.
Tukio la ubaguzi wa rangi ni nni?
Kwa madhumuni ya rasilimali hii, tukio la ubaguzi wa rangi ni kitendo chochote cha kauli au uchokozi wa kimwili, unyimwaji wa huduma, vitisho au kubaguliwa kwa misingi ya rangi ya mwili na/au asili ya kitamaduni.
Lini kupiga simu
Wapigie kitengo usaidizi wa simu kama umekumbwa au umeshuhudia tukio la ubaguzi wa rangi—bila kujali muda gani umeshapita.
Inapatikana Jumatatu hadi Ijumaa 9:00 asubuhi hadi 5:00 jioni (PT). Kinapatikana kwa kila mtu ndani ya British Columbia, bila kujali hadhi yako ya uhamiaji.
Kitengo cha Usaidizi wa Simu kwa Matukio ya Ubaguzi wa Rangi siyo ya kuitia dharura. Ikiwa uko katika shida ya haraka au hatari, piga simu 911.
Simu baada ya saa za kazi
Ikiwa uko katika shida ya haraka au hatari, piga simu 911.
Ikiwa unahitaji msaada tofauti na dharura baada ya saa za kazi, tafadhali acha ujumbe wa sauti na tutakupigia siku ya kazi ifuatayo.
Tafadhali kumbuka kuwa hatuachi ujumbe wa sauti kwa sababu ya masuala ya faragha na usiri, lakini kama ukituachia ujumbe, tutajitahidi kukutafuta mara kadhaa. Ikiwa hatutakupata kwenye simu, tafadhali tutafute tena.
Ikiwa uko katika shida ya haraka au hatari, piga simu 911.
Ikiwa unahitaji msaada tofauti na dharura baada ya saa za kazi, tafadhali acha ujumbe wa sauti na tutakupigia siku ya kazi ifuatayo.
Tafadhali kumbuka kuwa hatuachi ujumbe wa sauti kwa sababu ya masuala ya faragha na usiri, lakini kama ukituachia ujumbe, tutajitahidi kukutafuta mara kadhaa. Ikiwa hatutakupata kwenye simu, tafadhali tutafute tena.
Inatokea nini unapopiga simu
Unapopiga simu 1-833-457-5463, utaunganishwa moja kwa moja na mfanyakazi ambaye amemaliza mafunzo ya kukabili kiwewe na mafunzo ya unyeti wa kitamaduni.
Mpokea simu anaweza:
- Kusikiliza mapitio yako,
- Kukupa habari kuhusu huduma katika maeneo yako,
- Kukuongoza kwenye hatua zinazofuata kutegemea na daraja la faraja yako, na
- Kwa idhini yako, kukuelekeza kwa huduma zinazolingana vyema na mahitaji yako.
Usaidizi unapatikana katika lugha 240, hivyo mfahamishe anayepokea simu yako lugha ipi unayopendelea.
Tuko tayari kusaidia. Msaada uko hapa.
Bila malipo. Siri. Taarifa ya kiwewe
Maswali Yaulizwayo mara kwa mara
Ikiwa wewe au mtu mwingine unakabiriwa na hatari sasa hivi, tafadhali piga simu 9-1-1.
Matukio ya ubaguzi wa rangi hutokea kila siku katika kila ngazi ya jamii. Tupo hapa kutoa msaada na nyenzo za kukusaidia kukabiliana na athari za kinachotokea.
Tupo hapa kusaidia mtu yeyote ambaye amekutwa au kushuhudia tukio la ubaguzi wa rangi katika BC kwa sababu linaweza kuwa la kushangaza, kusikitisha, na kutenganisha.
Pia tunatoa msaada na rasilimali kwa watu wanaowasaidia wale ambao wamekutwa na tukio la ubaguzi wa rangi, kwa kuwa kushuhudia tukio hilo kwa njia isiyo ya moja kwa moja kunaweza pia kuathiri ustawi wako.
Kwa sasa huduma ya msaada inapatikana kwa kupiga simu 1-833-457-5463, Jumatatu hadi Ijumaa (isipokuwa sikukuu za kitaifa), saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni kwa saa za Pasifiki. Nje ya masaa ya kazi, wapiga simu wanaweza kuacha ujumbe na kutoa namba ya simu ili wapigiwe simu siku ya kazi inayofuata.
Tunatoa msaada kwa njia ya simu kwa yeyote aliyeko BC.
Wapokea simu wetu kwanza hujibu kwa kingereza. Kama unapendelea kuongea lugha nyingineyo, tafadhali mfahamishe mpokea simu wako na watamuunganisha mkalimani kwenye mazungumzo ya mfumo wa watu watatu. Ukalimani unatolewa na Voyce (orodha ya lugha haipo mtandaoni) au CanTalk (https://cantalk.com/our-languages/) na inapatikana katika zaidi ya lugha na lafudhi 240.
Lengo letu ni kukuunganisha na rasilimali zinazokutana na mahitaji yako hapo ulipo na kukupa msaada baada ya kukutwa au kushuhudia tukio la ubaguzi wa rangi.
Tunaweza kutoa rufaa kwa mashirika mbalimbali katika jimbo zima yaliyobobea katika kusaidia waathiriwa wa ubaguzi wa rangi, kujumuisha programu zinazotoa ushauri nasaha katika mazingira salama kwa tamaduni mbalimbali, vikundi vya misaada wa kijamii, elimu kuhusu kupinga chuki na utofauti, msaada wa kisheria, uhusiano wa kijamii, na mengine mengi.
Ndiyo, simu zote kwa huduma ya msaada ni siri. Taarifa zako binafsi hazitashirikishwa bila idhini yako, isipokuwa katika hali ambapo sheria inahitaji (kama vile kujidhuru au kudhuru mwingine), na kadhalika.
Taarifa binafsi hazitashirikishwa na vyombo vya usalama, isipokuwa katika wakati inahitajika na sheria (hatari ya kujidhuru au kudhuru mwingine), na kadhalika.
Huduma ya msaada inajitegemea kutoka vyombo vya usalama. Kama wewe au mtu mwingine uko kwenye hatari, tafadhali piga simu 9-1-1.
Ikiwa wewe ni mwathirika au shahidi wa uhalifu na ungependa kutoa ripoti kwa polisi, mpokeaji wa simu yako anaweza kukupa taarifa kuhusu hatua zinazofuata. Kupiga simu kwenye huduma hii ya msaada hakusababishi ripoti ya polisi, uchunguzi binafsi, usimamizi wa kesi, wala msaada wa haraka.
Ikiwa utatoa ripoti kwetu, taarifa tunazokusanya zinafanywa kuwa za siri (hazitakuonyesha moja kwa moja), zitawekwa pamoja kushirikishwa na Wizara ya Mwanasheria Mkuu wa BC. Lengo ni kusaidia kuelewa aina za matukio ya ubaguzi wa rangi yanayotokea BC; kusaidia, kuongoza, na kuboresha mipango, huduma, na juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi katika jimbo; na pia kusaidia kubaini mapungufu ya kimfumo ili serikali ya jimbo iweze kutekeleza mabadiliko ya maana hapa BC.
Kuna mashirika ya kijamii yaliyobobea katika kusaidia makundi maalum ya watu. Taarifa unazochagua kutoa kwa hiari zinatusaidia kukuelekeza kwenye huduma zinazokufaa na zinazopatikana kwa upande wako. Hii pia inatusaidia kuelewa kwa upana zaidi kile kinachotokea, nani anahitaji msaada, na aina gani ya msaada unahitajika katika maeneo mbalimbali ya BC. Una uhuru wa kuchagua taarifa gani utoe; bado tutakupa msaada bila kujali.
Tunashirikiana na mashirika ya kijamii ili kuhakikisha wapigaji simu wanapata msaada wa kuendelea, ikiwemo ushauri nasaha katika mazingira salama kwa tamaduni mbalimbali, warsha za huduma zinazozingatia athari za kiakili na kihisia, na msaada wa kisheria. Lengo letu ni kukuunganisha na msaada unaoendana na mahitaji yako maalum.
Taarifa kwa watoa huduma
Tunakaribisha mashirika ya kijamii, mashirika yanayoongozwa na watu wa asili na mataifa ya wenye ardhi jimboni kote ambao wamejikita kusaidia wale walioathiriwa na matukio ya ubaguzi wa rangi. Ili kujifunza zaidi kuhusu programu hii na fursa zake tembelea tovuti ya United Way BC.
Helpline Information and OpportunitiesKuhusu Kitengo cha Usaidizi wa Simu kwa Matukio ya Ubaguzi wa Rangi
Kitengo cha Usaidizi wa Simu kwa Matukio ya Ubaguzi wa Rangi ni rasilimali iliyo salama kiutamaduni na ni raslimali katika kutambua watu ambao wamewahi kushuhudia au kupatwa na kiwewe cha tukio la ubaguzi wa rangi, ambao hawataki au hawajui jinsi ya kuripoti polisi. Kitengo cha usaidizi wa simu kinahakikisha kuwa kila mmoja anaweza akapata maelezo na msaada wanaotaka na kuhitaji.
Simu zinapokelewa na wataalamu wajuzi ambao watasikiliza na kutoa maelezo na rufaa kwa mashirika ya kijamii kote kwenye jimbo yaliyojikita katika kusaidia matukio ya ubaguzi wa rangi, Pamoja na kuhamasisha upingaji wa ubaguzi wa rangi, utofauti, usawa na ujumuishaji.
Takwimu kutoka kwenye vyanzo visivyo vya wazi zilizokusanywa na kitengo cha Usaidizi wa Simu kwa Matukio ya Ubaguzi wa Rangi zitakuwa sambamba na videkoze kutoka kwenye mikakati mingine kwenye jimbo la British Columbia ya upingaji wa ubaguzi wa rangi, kusaidia, kuongoza na kuimarisha programu za jimbo za kupinga ubaguzi wa rangi, huduma na mikakati.
Kitengo cha Usaidizi wa Simu kwa Matukio ya Ubaguzi wa Rangi kiliundwa na inasimamiwa na tawi la Tamaduni nyingi na Upingaji wa Ubaguzi wa Rangi katika wizara ya Mwanasheria Mkuu, kwa ushirikiano na United Way ya British Columbia, na kufanya kazi na mashirika maalum ya kijamii kote jimboni B.C.
Tusaidie kutumikia jumuiya jimboni kote.
Fomu hii ni kwa ajili ya maoni tu. Ikiwa ukipenda kuongea na mtaalamu kuhusu tukio la ubaguzi wa rangi au kuunganishwa na huduma za usaidizi, piga simu 1-833-HLP-LINE (457-5463).